Shirika la Kimataifa la hisani la Save the Children, limesema takriban watoto 500 wamefariki kutokana na njaa nchini Sudan, wakiwemo watoto zaidi ya 20 katika kituo cha watoto yatima kinachosimamiwa na serikali katika mji mkuu Khartoum, tangu mapigano yalipozuka nchini humo mwezi Aprili.

Mkurugenzi wa shirika la Save the Children nchini Sudan, Arif Noor amesema hawakutegemea kuwaona watoto wakifa kwa njaa katika idadi na hali kama hiyo na kwamba wameshuhudia watoto wakifa njaa inayoweza kuzuilika kabisa. Amesema idadi ya watoto walioachishwa shule nchini Sudan pia imeongeza.

Shirika hilo pia lilisema kuwa karibu watoto 31,000 wanakosa huduma ya lishe na matibabu ya utapia mlo tangu kusitisha shughuli zake kwenye vituo 57 vya lishe nchini Sudan.

Mzozo huo wa Sudan, umegeuza jiji la Khartoum na maeneo mengine ya mijini kuwa viwanja vya vita huku wakazi wengi wakiishi bila maji na umeme, na mfumo wa huduma za afya nchini humo umeharibika.

Kaze: Namungo FC itakuwa bora Ligi Kuu
Serikali kuendeleza udumishaji wa Demokrasia Nchini