Mashambulizi ya Israeli katika ukanda wa Gaza yameshawauwa zaidi ya watu 2,200 tangu Hamas ilipovamia Israel wiki moja iliyopita. Wizara ya afya ya Gaza imesema watoto 724 na wanawake 458 ni miongoni mwa wahanga.

Takwimu hizo, zimetolewa baada ya taarifa ya awali iliyosema kuwa watu wasiopungua 324 wameuwawa kwa saa 48 zilizopita kutokana na mashambulizi yanayoendelea.

Jeshi la Israel limetoa taarifa hiyo na jana Jumamosi Oktoba 14, 2023 limesisitiza kuwa Wakazi wa Gaza wanalazimika kuondoka eneo la Kaskazini mwa mji huo kabla ya kuanza kwa mashambulizi.

Msemaji wa jeshi la Israel – IDF, Richard Hecht naye aliongeza kuwa upo muda salama wa kuondoka kwenye mji huo ambao ni kati ya saa nne asubuhi na saa kumi jioni kuelekea katika Pwani ya Gaza iliyo umbali wa kilometa 40.

Wahimizwa mazoezi kuepuka magonjwa nyemelezi
Habari Kuu kwenye Magazeti ya leo Oktoba 15, 2023