Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga linawashikilia vijana wawili wenye umri wa miaka 14, wote wakazi wa mtaa na kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga kwa tuhuma za kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka Sita(jina limehifadhiwa).

Kamanda wa Polisi Mkoani Shinyanga ACP Debora Magiligimba,amesema kuwa vijana hao walimlaghai mtoto huyo kwa pipi na kumpa hela kisha kumpeleka Kichakani karibu na eneo analoishi na wazazi wake kisha kisha kumfanyia unyama huo.

Mama mzazi wa mtoto aliyebakwa ndiye aliyebaini kubakwa kwa mwanaye na kutoa taarifa kituo cha polisi ambapo walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao.

Hata hivyo Jeshi la Polisi limesema kuwa watawafikisha mahakamani watuhumiwa hao mara baada ya upelelezi kukamilika na hatua kali za kisheria zitachukuliwa.

Trump, Biden mdahalo usio rasmi.
JPM kumalizia kampeni kaskazini