Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto – UNICEF, limesema mafuriko, dhoruba, ukame na mioto vimepelekea watoto milioni 43.1 katika baadhi ya Mataifa Duniani kuyahama makazi yao kati ya mwaka 2016 na 2021.
UNICEF imeonya kuwa hataua hiyo ni mwanzo na kusema inachochewa na ongezeko la joto Duniani, ambapo sehemu zilizokumbwa zaidi na kadhia hiyo ni Ufilipino, India, China, Canada na Marekani.
Aidha, imesema makadirio ya muda yanaonesha kuwa mafuriko yanayohusishwa na mito kuvunja kingo zake, yanaweza kupelekea Watoto milioni 96 kuyahama makazi yao katika miaka 30 ijayo.
Kuhusu Vimbunga, UNICEF imesema vyemyewe vinakadiriwa kuwa vitawahamisha watoto milioni 10.3, huku dhoruba ikiwahamisha Watoto milioni 7.2.