Maafisa wa serikali ya jimbo la Kaskakazini mwa Nigeria wamethibisha kutekwa nyara kwa watoto 136 na kwamba wameanzisha mawasiliano na wateka nyara katika juhudi za kuwakomboa.

Watoto hao wa shule miongoni mwao wakiwemo wenye umri wa miaka mitano walitekwa nyara wakiwa shuleni na watu waliokuwa na silaha kwenye jimbo la kaskazini mwa Nigeria. 

Mmiliki wa shule husika ameliambia shirika la habari la AP kwamba watu hao waliokuwa na silaha wakiwa wamepanda pikipiki waliivamia shule yake na kumuua mtu mmoja na pia kuwachukua kwa nguvu walimu watatu. 

Hii ni kadhia nyingine katika mfululizo wa watoto kushikiliwa kwa ajili ya kudai fedha nchini Nigeria

Naye Mmiliki wa Shule Umar Idris amesema kuwa idadi hiyo ya watoto inaweza ikaongezeka kwasababu maafisa bado hawajamaliza kuzungukia nyumba za wazazi wote kuuliza kama wamerudi nyumbani

Rais Samia aagana na Balozi wa China
Aweso aagiza aliyeidhinisha mradi wa maji yenye chumvi kuondolewa kazini