Mtoto wa gwiji wa soka nchini Ghana, Abedi Ayew Pele, Jordan Ayew ametimiza ndoto za kucheza soka nchini Uingereza baada ya kukamilisha usajili wa kujiunga na klabu ya Aston Villa akitokea nchini Ufaransa alipokuwa akiitumikia klabu ya Lorient.

Ayew, mwenye umri wa miaka 23, amekamilisha mpango huo kwa kukubali kusiani mkataba wa miaka mitano kuitumikia The Villans ambayo imemsajili kwa paund million 8.5 ambazo ni sawa na Euro million 12.

Mshambuliaji huyo anajiunga na wachezaji wengine waliojiunga na Aston Villa wakitoka nchini Ufaransa kama Jordan Amavi pamoja na Idrissa Gueye.

Kutokana na mpango huo kukamilishwa, watoto wote wa gwiji wa soka nchini Ghana Abedi Ayew Pele wataonekana katika ligi ya nchini Englnd msimu ujao, baada ya Andre Ayew kujiunga na klabu ya Swansea city mwanzoni mwa mwezi uliopita.

Andre alijiunga na Swansea city akitokea nchini Ufaransa alipokua akiitumikia klabu ya Olympique de Marseille.

Jordan ameondoka nchini Ufaransa huku akiwaachia kumbu kumbu mashabiki wa klabu ya Lorient kwa kuifungia klabu yao mabao 12 katika michezo 29 aliyocheza msimu uliopita.

Perez Na Ramos Wamalizana, Sasa Mambo Shwari
Lowassa Ashindilia Msumari Wa Richmond Baada Ya kuingia Chadema