Watoto wanne wamefariki dunia, baada ya ukuta wa Kanisa moja la Kipentekoste kuporomoka na kuwaangukia, huku watu  wengine 15 wakijeruhiwa kufuatia mvua kubwa iliyonyesha eneo la kusini mwa Taifa la Burundi.

Kwa mujibu wa Afisa wa Serikali wa eneo hilo, Esperanto Inarukundo amesema Mvua hiyo kubwa iliyoandamana na upepo mkali, ilianza kunyesha eneo la Kiyange majira ya saa moja asubuhi Oktoba 15, 2023.

Amesema, ” kulikuwa na hali mbaya ya hewa na ilisababisha uharibifu mkubwa, ikiwa ni pamoja na kuporomoka kwa Kanisa la Kipentekoste la Kiyange na hao watoto walikuwa wakihudhuria madarasa ya elimu ya Dini katika Shule ya Jumapili.”

“Tunaendelea na upekuzi kwenye vifusi na tayari tumegundua miili ya watoto wanne waliokufa na majeruhi 15 Kanisani, lakini tayari Shirika la Msalaba Mwekundu la Burundi na Idara ya Ulinzi wa raia walikuwa wakisaidia shughuli ya uokoaji,” alisema Inarukundo.

Rais Samia asisitiza uchukuaji tahadhari Mvua za El-Nino
Habari Kuu kwenye Magazeti ya leo Oktoba 16, 2023