Jeshi la kujenga Taifa – JKT, limesema litaendelea kushirikiana na jamii na hasa wahitaji wa vitu mbalimbali ikiwemo kuwapatia vyakula ili waweze kukabiliana na upungufu walionao wa vitu mbalimbali.
Kauli hiyo ya JKT imetolewa na Brigedia Jenerali, Hassan Mabena wakati akikabidhi Mchele, Maharagwe na mbuzi kwa ajili ya kitoweo katika makao ya Taifa ya watoto kilichopo kikombo Mkoani Dodoma.
Matumizi ya Teknolojia: JKT liwekeze kwa Vijana – Dkt. Mpango
Amesema, vyakula hivyo vilivyotolewa na Jeshi ni sehemu ya mavuno yao kwa mwaka 2023 na itawasaidia watoto hao kujikimu.
Akizungumza mara baada ya kupokea vyakula hivyo, Kamishna MsaidiziUustawi wa Jamii toka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Tullo Masanja ameitaka jamii kujitokeza kuwasaidia watoto hao.
Msaada huo ni sehemu ya matukio ya sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya JKT, kabla ya kuhitimishwa kwake Julai 10 2023.