Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga linawashikilia watu 11 kwa tuhuma za kumshambulia na kumuua mtu mmoja aliyetuhumiwa kuiba pikipiki Wilaya ya Korogwe.

Akizungumza kuhusu na tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Blasius Chatanda, amesema Marehemu alituhumiwa kuiba pikipiki Korogwe Tanga, Julai 27 2021, na kutokomea nayo kusikojulikana.

RPC Chatanda amesema Baada ya kufanya tukio hilo, Madereva bodaboda wa eneo aliloiba pikipiki hiyo walianza kufanya msako na baada ya siku chache walimkamata akiwa na pikipiki hiyo kisha wakampiga.

“Baada ya kumkamata walianza kumshambulia kwa vipigo kisha kumfunga kamba kwenye pikipiki na kuanza kumburuza barabarani (barabara ya vumbi). Hata hivyo, kutokana na majeraha makubwa aliyoyapa, mtu huyo alifariki dunia,” Amesema RPC Chatanda

Aidha Jeshi la Polisi limewakamata watu 11 kwa kwa ajili ya uchunguzi kuhusika na tukio hilo la kinyama, Uchuguzi utakapo kamilika watuhumiwa hao watapfikishwa Mahakamani.

Sambamba na hayo yote RPC Chatanda amewahasa wanachi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mikononi mao kwani kwa kufanya hivyo ni ukiukwaji wa sheria.

Gazeti la Uhuru lapewa onyo
Watu wa familia moja wafariki dunia kwa kula sumu waliodhani ni chumvi