Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema kwamba limepokea taarifa ya kutokea vifo vya watu 12 hadi sasa vilivyotokana na athari ya mvua zinazoendelea kunyesha Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na wandishi wa habari, kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa thibishisha kutokea kwa vifo hivyo katika mikoa ya kipolisi ya Ilala na Kinondoni

“Jeshi la polisi limepokea taarifa ya vifo vya watu 12 vilivyotokana na mvua za Mafuriko yalishuhudiwa na kutokana na hali hiyo, mkoa wa kipolisi ulioathirika sana ni Ilala ukifuatiwa na Kinondoni” amesema Kamanda Mambosasa.

Mambosasa, amesema kuwa watu nane walikufa katika Mkoa wa Kipolisi Ilala na wa nne kutoka Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni wakiwemo watoto wawili wa familia moja.

“Watoto hao walifariki kwa kusombwa na maji baada ya nyumba yao iliyopo katika bonde la Kigogo kujaa maji na watoto hao kushindwa kujiokoa,”.

Aidha jeshi hilo limewataka wananchi kuwalinda watoto pamoja na kuchukua taadhari kwa kuama maeneo ya mabondeni.

Producer S2Kizzy avamiwa na kupigwa
Antoine Griezmann azidi kupaa Ufaransa