Watu 13 wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa vibaya mara baada ya ukuta wa kanisa walilokuwa wakisali kuanguka.
Tukio hilo limetokea Afrika kusini katika mji wa KwaZulu – Natal wakati wa ibada ya pasaka ya Ijumaa kuu kufanyika katika kanisa la Pentekoste.
Imeripotiwa watu 16 wamejeruhiwa vibaya na kukimbizwa hospitali kwa matibabu ya haraka na majeruhi wengi wametajwa kuwa ni wanawake.
Polisi wameongezea kuwa wengi wao walikuwa ni vijana wadogo mmoja akitajwa kuwa na umri wa miaka 11.
Adha hiyo imetajwa kutokea kutokana na upepo mkali kuvuma na mvua kali zilizonyesha usiku wa Alhamisi.
Ukuta huo wa mbele ya kanisa ulianguka wakati misa ikiwa inaendelea.
Rais wa nchi hiyo Cyril Ramaphosa mwaka jana alitembelea kanisa hilo hivyo wametumia fursa hiyo kumuomba awasaidia kujenga upya kanisa hilo.