Watu 14 wamefariki dunia papo hapo na watatu kujeruhiwa Mkoani Singida, kufuatia ajali ya barabarani iliyohusisha gari ndogo aina ya Hiace na Lori kugongana uso kwa uso Ikungi mkoani humo.

Akizungumza Leo Desemba 14, 2020 Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Singida Sweetbert Njewike amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyohusisha gari aina ya Hiace iliyokuwa ikitokea mkoani Mwanza na Lori lililokuwa linatokea Dar es Salaam kuelekea Kahama.

Kamanda Njewike amesema chanzo cha ajali hiyo ambayo imesababisha vifo vya wanaume saba na wanawake saba ni dereva wa gari ndogo kutaka ‘kuovateki’ lori bila kuchukua tahadhari yoyote.

Majeruhi wanatibiwa katika hospitali ya wilaya ya Manyoni na miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika Hospitali ya mkoa wa Singida.

Aidha, Kamanda Njewike ametoa wito kwa madereva kuhakikisha wanazingatia sheria za usalama barabarani.

Biteko aanza kutumbua majipu
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Desemba 14, 2020