Watu 14 wameuwawa na wengine 14 wamejeruhiwa katika mji wa San Bernadino, Mashariki mwa Los Angeles, katika shambulio lililofanywa na watu watatu wenye silaha waliovalia kijeshi.

Kwa mujibu wa ripoti ya polisi wa San Bernadino, tukio hilo limetokea katika kituo cha huduma kwa watu wenye ulemavu na kwamba wahusika walifanikiwa kutoroka kwa gari.

Silaha zilizotumika zinadaiwa kuwa silaha kubwa za masafa marefu. Mkuu wa kituo hicho cha watu wenye ulemavu palipotokea mauaji hayo ya kinyama anasema milio ya risasi ilisikika katika jengo lililokodishwa kwa ajili ya hafla iliyoandaliwa na Idara ya Afya.

Rais wa Marekani, Barack Obama amelielezea tukio hilo kuwa tukio la kusikitisha na kwamba hilo ni tukio la mauaji ya watu wengi ambalo halifanani na tukio lingine lolote duniani.

Tukio hilo limeongeza mvutano wa kuruhusu au kubana umiliki wa silaha nchini Marekani. Inadaiwa kuwa Marekani ni nchi ambayo silaha zinapatikana kwa urahisi zaidi na watu wengi wanamiliki silaha hizo.

Mahakama Yamtia Hatiani Oscar Pistorius, Anaweza Kwenda Jela Miaka 15
Ripoti: Bilionea wa ‘Unga’, El Chapo alifanya Mapenzi Gerezani Mara 46 kabla ya kutoroka