Watu 16 wamefariki Dunia na wengine 32 kujeruhiwa baada ya basi la Ahmeed lenye namba za usajili T 732 ATH lilokuwa likitokea Mbeya kwenda Tanga kugongana uso kwa uso na lori lenye namba IT 2816.

Katika ajali hiyo, watu kadhaa wamejeruhiwa wakati lori lilikuwa likitokea Dar es Salaam kwenda DR Congo kugongana uso kwa uso na basi la kampuni ya Ahmeed

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fortunatus Muslim amesema ajali hiyo imetokea jana march 18, majira ya saa 10.30 jioni na kusababisha vifo vya watu 16.

Kamanda Muslim amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa lori hilo kujaribu kumkwepa mwendesha pikipiki maarufu bodaboda hivyo, kupoteza mwelekeo na kukutana na basi hilo uso kwa uso.

Kwa mujibu wa Kamanda Muslim, basi hilo lilikuwa likitokea Mbeya kwenda Dar es Salaam. Miili ya marehemu hao imehifadhiwa kwenye Hospitali ya Mkoa wa Morogoro huku majeruhi wakiendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo.

Hata hivyo, Kamanda Muslim ametahadharisha kuwa idadi ya vifo inaweza kuongezeka kwa kuwa, kazi ya uokoaji bado inaendelea kwenye eneo hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Martine Shigela, ameonya madereva kutumia barabara kwa kuzingatia sheria za barabarani.

“Hii ajali inaonekana madereva wote walikuwa na mwendo mkali, barabara hii ni kubwa na inatumiwa na idadi kubwa ya magari kwa kuwa inaunganisha na nchi jirani hivyo, ni muhimu kwa madereva kuwa makini” amesema RC Shigela

Vita Ukraine matumizi mabaya ya madaraka - Papa Francis
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Machi 19, 2022