Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi limewakamata watu 19 kwa tuhuma za uvunjaji wa nyumba na wizi wa vitu mbalimbali vya matumizi ya nyumbani, katika oparesheni ya siku tatu ya kuondoa vibaka iliyofanyika katika manispaa ya mpanda.
Akitoa taarifa kwa mkuu wa mkoa wa Katavi; Kamanda wa Polisi mkoa Benjamin Kuzaga amesema wamefanya operesheni maalum ya siku tatu na kubaini watu hao wanashirikiana na wa mikoa jirani Kigoma na Tabora katika uuzaji wa vitu hivyo.
Baadhi ya vitu vilivyopatikana katika msako huo ni pamoja na runinga, radio, feni, sofa set, pikipiki, magodoro, rice cooker, majiko ya gesi na jenereta.
Kamanda Kuzaga amesema kuwa kati ya watuhumiwa 19 waliokamatwa watu 15 wamekamatwa katika manispaa ya Mpanda na wengine wanne wamekamatwa katika mikoa ya Tabora na Kigoma
“Tumekata chain hii nzima nab ado tunaendelea mpka mkoa wa Rukwa, lengo kubwa ni kuhakikisha mji wetu unakuwa na Amani na hawa walioshindwa tabia wanavuruga maendeleo ya wananchi tutahakikisha tunawakomesha” Amesema Kamanda kuzaga.
Aidha watuhumiwa wote watafikishwa Mahakamani ili sharia ichukue mkondo wake dhidi yao.
Sambamba na hayo yote Kamamnda Kuzaga amekemea tabia ya kuficha wahalifu na kutoa wito kwa jamii kutoa taarifa ili kusaidia kukomesha tabia za wizi.