Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja linawashikilia watu 20 kwa tuhuma za kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Hassan Nassir Ali ambapo amesema kuwa wamewakamata watu hao wakipatiwa mafunzo ya namna ya kuzitambua haki zao yaliyokuwa yakitolewa na taasisi iliyotambulika kwa jina la Bridge Initiative.

“Jeshi la Polisi limewakamata vijana 20 wenye umri chini ya miaka 18 wakijihusisha na mapenzi ya jinsi moja, kati ya hao wanawake ni 12 na wanaume nane. Tunaendelea kuwafanyia uchunguzi na kuwahoji vijana hao, jeshi la polisi halitafumbia macho vitendo hivyo ambavyo vinakwenda kinyume na maadili ya nchi,” amesema Kamanda Hassan

Hata hivyo, kwa upande mwingine, hatua hiyo imekuja mara baada ya kutolewa kauli na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mahamoud ya kutaka kukomesha vitendo hivyo mara moja ambavyo vimekuwa vikitoa sifa mbaya katika mkoa huo.

BAVICHA walibipu jeshi la polisi, wasema maombi yako palepale
Magazeti ya Tanzania leo Septemba 17, 2017