Takriban watu 24 wamefariki dunia na wengine 79 kujeruhiwa baada ya sehemu ya barabara ya juu (flyover) kuporomoka na kusababisha treni ya abiria kuanguka katika barabara ya chini iliyokuwa na watu wengi nchini Mexico.

Kwa mujibu wa taarifa, waokoaji walilazimika kushikilia sehemu ya treni hiyo kwa kreni ili kuwaokoa abiria waliokuwa wamekwama ndani ya kifusi.

Katika ajali hiyo, watu 79 wamejeruhiwa na 49 kati yao ambao wapo mahututi wamepelekwa katika hospitali Mexico City.

Taarifa za Serikali zimeeleza kuwa miili ya watu watano pekee ndio imetambuliwa.

Barabara hiyo ya juu imewahi kulalamikiwa kwa kujengwa chini ya kiwango baada ya kukamilika kwake mwaka 2013.

Mamlaka nchini humo bado zinaendelea na uchunguzi kuhusu chanzo cha ajali hiyo mbaya huku barabara ikifungwa.

Ninja: Miquissone ajipange
Teddy Mapunda afariki dunia