Watu 30 pekee ndiyo watakaoshiriki mazishi ya aliyekuwa mume wa Malkia Elizabeth II wa Uingereza, Mwanamfalme Philip.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na kasri ya Buckinham, ibada ya mazishi inatarajiwa kuanza saa tisa alasiri, sawa na saa 11 jioni kwa Afrika Mashariki kesho Jumamosi, Aprili 18, 2021.

Watu wote 30 watakaoshiriki ni ndugu wa karibu wa Malkia Elizabeth na mumewe Mwanamfalme Philip. Orodha hiyo ya wageni inaongozwa na Malkia mwenyewe na watoto wake wanne.

Pia watakuwepo wenza wa watoto wa Malkia, mke wa Mwanamfalme Chalres, Camilla Duchess wa Cornwall, mume wa Bintimfalme Anne Bw. Timothy Laurence na mke wa Mwanamfalme Edward Sophie Countess wa Wessex.

Wengine ni wajukuu wa Malkia na Mwanamfalme Philip wakiongozwa na Mwanamfalme William pamoja na mkewe Kate Duchess wa Cambridge, Mwanamfalme Harry, Bintimfalme Beatrice na mumewe Edoardo Mapelli Mozzi, Bintimfalme Eugenie na mumewe.

Jack Brooksbank, Peter Phillips, Zara Tindall na mumewe Mike Tindall, Lady Louise Windsor na Viscount Severn.

Wengine ni ndugu wa karibu wa familia hiyo wakiwemo watoto wa aliyekuwa mdogo wake Malkia Bintimfalme Margaret; Earl wa Snowdon, Lady Sarah Chatto na mumewe Daniel Chatto. Ndugu wengine ni Mtawala wa Gloucester, Mtawala wa Kent, Bintimfalme Alexandra na Countess Mountbatten wa Burma.

Ndugu wa Mwanamfalme Philip kutoka Ujerumani ni; Bernhard, Mwanamfalme wa Baden, Mwanamfalme Donatus wa Hesse na Mwanamfalme Philipp WA Hohenlohe-Langenburg.

Mdee aibua mapya madeni ya mifuko ya hifadhi
Ndugai aonya wabunge kutumia usafiri wa bodaboda