Watu 41 wakiwemo watoto wawili na mhudumu mmoja wa ndege wamefariki dunia baada ya ndege ya Urusi kutua kwa dharura na kulipuka moto katika uwanja wa ndege wa Sheremetyevo mjini Moscow, jumapili ya Mei 5, 2019.

Waziri wa Afya wa Moscow, Dmitry Medvedev amezungumza na vyombo vya habari na kusema kuwa Katika ajali hiyo watu 37 wamenusurika kifo na wengine 11 wamejeruhiwa vibaya.

Vyombo vya habari Russia vimeripoti kuwa ndege hiyo ilikuwa inatoka Moscow kuelekea Murmansk ikiwa imebeba abiria 78 iliamua kugeuza na kutua uwanja wa ndege wa Sheremetyevo mjini Moscow baada ya mawasiliano kukatika kutokana na radi kali zilizopiga.

Video katika mitandao ya kijamii zinaonyesha baadhi ya abiria wakitumia mlango wa dharura kutoka kwenye ndege hiyo ya Aeroflot iliyokuwa inateketea moto.

Aidha, sababu ya ndege hiyo kuwaka moto bado haijafahamika uchunguzi zaidi unaendelea kubaini chanzo kilichopelekea ndege hiyo kuwaka moto na kusababisha vifo vya watu na wengine kujeruhiwa vibaya.

 

Video: Kopa Fasta yaneemesha wasanii Mwenge
Video: Stori ya Kamchape wa Mwenge kuhusu Kitambulisho cha TACIP kilivyomsaidia