Rais wa Marekani Joe Biden amesema kuwa uwekezaji mkubwa unahitajika nchini humo baada ya mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali kuua watu 41 kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo.
Ametoa taarifa hiyo baada ya mvua kubwa na kimbunga kilicho athiri majimbo ya New Jersey na New York, huku baadhi ya wakazi wakiwa wamekwama katika maeneo ya chini ya nyumba zao yaliyofurika maji.
“Marekani inakabiliwa na uharibifu unaotokana na hali ya hewa kote nchini.” Amesema Biden.
Aidha Gavana wa jimbo la New Jersey Phil Murphy amesema kuwa takribani watu 23 wamefariki Dunia kwa maji katika jimbo hilo wengi wao wakiwa ndani ya magari,
Ambapo katika jimbo la New York City, watu takribani 14 wamepoteza maisha akiwemo mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka miwili.