Watu wenye silaha wamewauwa raia 56 na kujeruhi wengine 20 Januari 02 2021, katika shambulizi linaloshukiwa kuwa la kigaidi nchini Niger.

Waziri wa Mambo ya Ndani Alkache Alhada amesema shambulizi hilo lilitokea katika vijiji vya Tchombangou na Zaroumdareye karibu na mpaka na Mali.

Shambulizi hilo limetokea wakati Niger ikihesabu kura za uchaguzi wa Desemba 27, 2020 ambapo mpaka jana, matokeo yaliyotangazwa yanaonyesha chama tawala cha Demokrasia na Ujamaa kinaongoza viti vya bunge.

Uchaguzi wa rais utaingia katika sehemu ya pili mwezi Februari baada ya kutopatikana mshindi wa moja kwa moja, Mgombea wa chama tawala Mohamed Bazoum alipata asilimia 39.6 ya kura na mgombea wa upinzani Mahamane Ousmane akipata asilimia 16.9.

Taifa hilo linatarajiwa kwa mara ya kwanza tangu kupata uhuru mwaka 1960 kutoka Ufaransa, kukabidhiana madaraka kwa njia ya kidemokrasia

Biashara zitakazo toa huduma kwa siku 30
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Januari 3, 2021.