Watu sita wa Kijiji cha Nguyami, Kata Idibo Wilaya ya  Gairo mkoani  Morogoro wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kufukua kaburi la marehemu aliyefahamika  kwa jina la Rehema  Michael.

Akizungumza na kituo cha habari cha mtandaoni cha Dar24, Kamanda wa polisi Mkoa wa Morogoro Fortunatus Musilimu amesema kuwa mpaka sasa wanaendelea na kufanya upepelezi na kuwahoji watuhumiwa hao kuhusiana na tukio hilo.

Amesema kuwa wanashirikiana na wananchi kwa kuitisha Mkutano wa hadhara kujadili suala hilo ambapo Mkutano huo umedhulumiwa na viongozi mbalimbali kuanzia ngazi ya Mkuu wa Wilaya mpaka Mwenyekiti wa mtaa na viongozi wa kidini ili kujua maoni yao na kupanga mikakati ya kukabili swala hilo huku wanachi wakiliomba jeshi la polisi hatua kali zichukuliwe juu ya wahusika watakaobainika.

Aidha, Kamanda Musilimu amewaomba wananchi kutoa ushirkiano wa hali na mali kwa jeshi la polisi endapo watakuwa na taarifa yoyote kuhusiana na tukio hilo.

Kamanda Musilimu amesema kuwa uchunguzi utakapokamilika wahusika wote watapelekwa mahakamani na sheria itachukua mkondo wake dhidi yao.

Sambamba na hayo yote kupitia mkutano huo jeshi la polisi limetoa elimu kwa wananchi kuachana na imani potofu za kishirikina za kutumia viungo vya binadamu.

Ajinyonga kwa tuhuma za kuiba Shilingi 5000
UEFA yathibitisha Conference League