Takribani watu 60 wameuawa, katika mapigano makali kati ya makundi mawili hasimu, Kusini mwa nchi ya Libya.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na msemaji wa kundi la ‘Libyan National Army’, zimeeleza kuwa uwanja wake wa ndege wa Brak al-Shati, ulivamiwa, ambapo kundi moja linalojiita Third Force, linasemekana kutekeleza shambulio hilo.
Katika eneo hilo kumekuwa na uangazi mkubwa kutokana na taharuki inayotanda kati ya wanaounga mkono Serikali inayotambuliwa na Umoja wa mataifa iliyoko katika mji mkuu Tripoli, na wapinzani wao.
Aidha, Kamanda mkuu wa Libyan National Army, Khalifa Haftar mapema mwezi huu alikutana na kiongozi mkuu wa Serikali iliyopo Tripoli, Fayez al-Sarraj, ili kujaribu kuzima uhasama unaotokota Kusini mwa nchi hiyo.