Watu 63 wamefariki dunia na wengine 182 wamejeruhiwa vibaya katika mlipuko wa shambulio la bomu la kujitoa muhanga, uliotokea katika sherehe ya harusi katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul.

Shambulio hilo limetokea huku kundi la Taliban pamoja na serikali ya Marekani wakiwa wanajaribu kujadili makubaliano ya Marekani kuondoa vikosi vyake vya kijeshi nchini Afghanistan, ili kundi la Taliban lifanye mazungumzo ya kutafuta amani na serikali ya Afghanistan ambayo inaungwa mkono na Marekani.

Kundi la Taliban limekataa kuhusika na shambulio hilo na limelaani vikali kwa waliohusika.

Aidha, shambulio hilo limetokea magharibi mwa mji wa Kabul kwenye idadi ndogo ya Washia, katika ukumbi wa harusi uliokuwa umejaa watu waliokuwa wakisherehekea harusi hiyo.

Kwa upande wake Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani wa Afghanistan, Nasrat Rahimi, amesema kuwa miongoni mwa waathirika ni wanawake na watoto.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Agosti 19, 2019
Idadi ya waliofariki kwenye ajali ya moto Morogoro yaongezeka