Jeshi la polisi mkoani Morogoro linawashikilia majambazi saba waliokamatwa na pikipiki tisa na bajaji moja zinazodhaniwa kuwa zimeibiwa jijini Dar es salaam.
Watuhumiwa hao walikamatwa katika msako maalumu uliofanyika kwa siri katika Taarafa ya Ruhembe wilayani Kilosa.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Selemani Katumbala, Mashauri Mlinda, Danford Chengula, Emmanuel Dickson, Simon Gerard, Musa Mohamed na Abdallah Rashid.
Matei amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa katika matukio tofauti kuanzia kipindi cha mwishoni mwa mwaka jana hadi januari 2018.
-
Kigwangalla: Najitoa kupigania maliasili zetu natukanwa na kushambuliwa
-
Burundi yapingana na takwimu za UNHCR
Ameongezea kuwa msako huo umefanyika baada ya kuwepo kwa taarifa zilizotolewa na raia wema kuhusu pikipiki hizo ambazo zilikuwa zikimilikiwa na watuhumiwa hao.
Aidha Kamanda Matei amesema kuwa watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.