Karibu watu 75 wamefariki dunia baada ya daraja kuporomoka nchini India, wakati ambapo karibu watu 500 walikuwa wakiadhimisha sherehe za kiimani za Diwali kwenye daraja hilo, na maeneo ya karibu wakati nguzo zilizokuwa zinalishikilia zilipokatika.
Waziri wa serikali ya mkoa wa Gujarat, linapopatikana daraja hilo, Brijesh Merja amesema pamoja na vifo hivyo, bado kuna wengine wengi waliozama majini na wengine 80 tayari wameokolewa.
Daraja hilo la Machchhu, lililojengwa karibu miaka 150 iliyopita lina urefu wa karibu kilomita 200 na lilifunguliwa siku ya Jumatano baada ya kufungwa kwa miezi saba kwa ajili ya matengenezo.
Hata hivyo, lilifunguliwa kabla ya kupata cheti cha idhini ambapo Waziri mkuu wa India, Narendra Modi ametangaza familia za wahanga kulipwa, wakati operesheni za uokozi zikiendelea.