Naibu Waziri Wizara ya Maliasili na Utalii Mary Masanja amesema kuna zaidi ya watu milioni mbili ambao wanasubiri ajira katika sekta ya utalii.
Masanja amezungumza hayo wakati akizindua programu ya kuwezesha mnyororo wa thamani wa ufugaji nyuki nchini.
Alisema kuwa Sekta ya Utalii nchini inakadiriwa kuajiri watu takribani milioni mbili katika mnyororo mzima wa thamani wa wafugaji nyuki.
Aidha, amesema katika kuhakikisha kuwa sekta ya ufugaji nyuki inachangia pato la Taifa, Serikali imeweka mikakati mbalimbali itakayowezesha sekta hiyo kuchangia katika kuongeza ajira kwa vijana na kinamama pamoja kuchangia kwenye pato la Taifa.
Wakati huo huo , amesema Wizara kwa kushirikiana na Kamisheni ya Umoja wa Ulaya kwa pamoja wameandaa program hiyo waliyoizundua kwaajili ya kuwezesha mnyororo wa thamani wa ufugaji nyuki ambao utagharimu euro milioni 10 sawa na fedha za kitanzania shilingi bilioni 27.
Programu itatekelezwa katika mikoa mitano ya Tanzania Bara ambayo ni Tabora, Kigoma, Katavi, Singida na Shinyanga na mikoa miwili ya Tanzania visiwani ambayo ni mkoa wa kusini Pemba na Kaskazini.