Watalaamu wanasema mvua zimekuwa kubwa mno mwaka 2019 kutokana na kile kinachoitwa Indian Ocean Dipole hali ambayo inasababisha viwango vya juu vya joto katika maji kwenye bahari ya Hindi na kupanda kwa digrii mbili celcius.
Nusu ya waliopoteza maisha tangu kuanza kwa msimu wa mvua ambao bado haujaisha ni kutoka nchini Kenya.
Wakati huohuo mvua kubwa zimesababisha mafuriko katika sehemu za Sudan Kusini na kuzilazimisha jamii ambazo ziliwahi kukoseshwa makazi kutokana na ghasia kuhama tena.
Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, tayari limepeleka chakula kupitisha shirika la hisani la Uingereza Oxfam, Lakini mwakilishi wa Umoja wa Mataifa kwa Sudan Kusini anasema kiwango kinachohitajika ni kikubwa mno kuliko ilivyo dhaniwa.
Ikumbukwe kuwa majira ya kunyesha mvua Afrika Mashariki kati ya October na December, lakini mwaka huu imenyesha kwa kiwango kikubwa, Wanasayansi wanalaumu wanasema ni kwa sababu ya viwango vya juu vya joto kwenye bahari ya Hindi. Na hivyo kupelekea maji kutoa mvuke na hatimaye kusababisha mvua nyingi kuliko kawaida.