Rais wa Benki ya Dunia (WB), David Malpass ameonya kuwa kutokana na janga la virusi vya corona watu takriban Milioni 60 wapo hatarini kukumbwa na umasikini mkubwa.
Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, umasikini mkubwa ni pale mtu anapotumia chini ya Dola za Marekani 1.90 (Tsh. 2,315) kwa siku.
Malpass amesema kuwa benki ya Dunia inategemea ukuaji wa uchumi duniani kushuka kwa 5% mwaka huu ambao mataifa mengi ulimwenguni yanakabilina na mlipuko wa ugonjwa wa Covid 19.
Benki ya dunia imesema inakadiria watu Milioni 60 watakumbwa na umasikini na makadirio hayo yatafuta jitihada zote zilizofanywa na Benki hiyo kwa miaka mitatu iliyopita.
Janga la virusi vya Corona tayari limesababisha biashara kufungwa na mamilioni ya watu kupoteza ajira ulimwenguni kote, huku nchi masikini zikiathirika zaidi.