Tetemeko la ardhi lenye nguvu ya 6.2 katika vipimo vya Richter limetokea katika eneo la Umbria katikati mwa Italia na kufukia watu chini ya vifusi.

Tetemeko hilo lilitokea muda wa saa tisa na dakika thelathini na saa sita usiku saa za Italia (01:36 GMT), 76 km (maili 47) kusini mashariki mwa mji wa Perugia, katika kina cha 10km (maili sita) chini ya ardhi, taasisi ya Marekani inayohusika na mitetemeko ya ardhi USGS imesema.

Mitetemeko imetokea katika miji ya mbali kama vile Roma na Italia. Mjini Roma, baadhi ya majumba yalitikisika kwa sekunde 20, kwa mujibu wa gazeti la La Repubblica.

Watu wanne wameripotiwa kufariki katika eneo la Accumoli, na meya wa mji jirani wa Pescara del Tronto amesema watu wawili wazee walifariki baada ya nyumba yao kuporomoka.

Eneo hilo, ambalo la mikoa ya Lazio na Marche, ni maarufu sana kwa watalii na kuna wageni wengi waliokuwa eneo hilo kipindi hiki cha shughuli nyingi za kitalii , Waziri mkuu wa Italia, Matteo Renzi, amesema serikali yake inaendelea kuwasiliana na taasisi za kiraia za ulinzi wa nchi hiyo.

“Barabara za kuingia na kutoka mjini hazipitiki. Nusu ya mji imeharibiwa. Watu wamefukiwa chini ya vifusi… kumetokea maporomoko ya ardhi na kuna daraja moja ambalo huenda likaporomoka,” alisema waziri mkuu.

 

Maneno Ya Mwambusi Baada Kipigo Cha 3-1 Dhidi Ya TP Mazembe
Mbwa Achaguliwa Tena Kuwa Meya Minnesota, Marekani