Watu 24 wa familia moja nchini Nigeria wamefariki baada ya kula chakula kinachoshukiwa kuwa na sumu, tukio hilo limetokea katika kijiji cha Danzanke jimbo la Sokoto, kaskazini magharibi mwa Nigeria

Kamishna wa Afya Ali Inname, amesema kuwa familia hiyo ilitumia kimakosa kemikali ya mbolea inayotambulika kwa jina la Gishirin Lalle  ambayo ilionekana kama chumvi wakati wa kuandaa chakula.

Hata hivyo taarifa zinasema kuwa watu wawili wa familia hiyo ambao walionja chakula hicho wanaendelea kupatiwa matibabu Hospitalini.

Kufuatia tukio hilo, maafisa wa afya wameshauri watu kuweka vitu vyenye sumu mbali na maghala yao ya chakula kwa sababu za usalama.

Watu 11 wakamatwa kwa tuhuma za mauaji
Jeshi la Polisi linamshikilia mbakaji aliyetumia mtindo wa teleza