Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro amesema Ofisi ndogo za NIDA iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Arusha imeibiwa vifaa vyote na Watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo.

Muro amesema kuwa wizi huo umefanyika kimtandao kwasababu ofisi ndogo za NIDA zipo karibu kabisa na jengo la NMB Bank na halmashauri ina walinzi wake.

Aidha ametaja vifaa vilivyoibwa ni pamoja na Kompyuta Mpakato nne na Kamera si chini ya tatu pamoja na vifaa vingine vilivyokuwa vikiingiza majina kwenye mifumo na ambapo amesema wizi huo unaonekana ni wa ndani kwani milango haikuvunjwa.

Ameongeza kuwa tukio hilo limewashtua na ni mara ya pili tukio kama hilo kutokea amapo mara ya kwanza lilitokea Ofisi za NIDA Makao Makuu Wilaya ya Arumeru na  baadhi ya vifaa viliibwa taratibu kwa muda mrefu.

Katika hatua nyingine  Jerry Muro amewaomba Wananchi kuwa, watulivu kwa kipindi hiki ambacho yeye na Kamati ya Ulinzi na Usalama wanaendelea kufuatia na vile vile ameeleza kuwa kwa sasa hakutakuwa na huduma katika Ofisi hiyo ya Halmashauri ya Arusha.

Mtoto wa miaka 1o ajitahiri kwa kisu
Vanessa mdee aja na 'show' mpya 2020

Comments

comments