Watu watatu wamefariki dunia huku wawili kati yao miili ikiwa imeteketea kwa moto katika ajali ya iliyohusisha lori la mafuta na gari dogo.
Katika ajali hiyo ambayo imetokea mkoani Mbeya, mmoja amabye ni mchungaji amefia hospitalini wakati akipatiwa matibabu katika hospital ya Mbeya,
Lori hilo la mafuta lilikua likitokea Jijini Dar es salaam na kuelekea nchini Zambia, liligonga gari dogo na kisha kulipuka moto katika eneo la old vwawa wilayani Mbozi Mkoani Songwe.
Akizungumzia tukio hilo mara baada ya kushiriki zoezi la uokoaji na kutoa mabaki ya miili ya marehemu kwenye magari, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Omary Mgumba ameelezea chanzo cha ajali hiyo ikiwa ni lori hilo kumshinda Dereva na kusasabisha kuligonga gari dogo
Amesema gari dogo lilikuwa limembeba Mwenyekiti wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo kuu la Mbeya, Willy Mwasile akiwa na familia yake ya watu watatu.
Kaimu kamanda wa polisi mkoani Songwe, Rashid Ngonyani amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ya lori la mafuta lenye namba za Usajili T980BCWA na trela lake namba T231 CWA mali ya kampuni ya Asas ya Iringa tukio ambalo limetokea jana tarehe 7.