Jeshi la Polisi Mkoani Njombe kwa kushirikiana na wananchi limefanikiwa kuwaua watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni majambazi huku mmoja akifanikiwa kutoroka kwa kutumia gari ndogo aina ya Spacial.

Akizungumza na vyombo vya habari makao makuu ya jeshi hilo mjini Njombe, kamishna msaidizi wa jeshi la polisi mkoani humo, Salum hamduni amesema watu hao wameuawa kwa kujaribu kufanya unyang’anyi wa kutumia silaha mjini Makambako mkoani Njombe.

“Mnamo tarehe 5/6/2019 majira ya saa 20:15 katika kituo cha kuuza mafuta kiitwacho Negelo kilichopo mtaa wa Kipagamo Kata ya Makambako, watu watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi jinsia ya kiume wenye umri kati ya 35-45 waliuawa wakati wa majibizano na askari polisi wakati walipovamia katika kituo hicho kwa lengo la kufanya unyang’anyi,”amesema kamanda Hamduni

Aidha, amesema kuwa jeshi la polisi kwa kushirikiana na walinzi wa kituo hicho cha mafuta waliweka mtego ndipo majira hayo wakafika watu hao wakiwa na gari dogo aina ya Spacial wakiwa wamezima taa huku wakiwa wameshika silaha ndogo kila mmoja.

Amesema kuwa watu hao walipo amriwa na askari walikaidi amri hiyo na kuanza kufyutua risasi ndipo askari walijibu mapigo na kufanikiwa kuwaua watu wawili na katika eneo la tukio kumekutwa na silaha aina mbili za shotgun/gobore ikiwa na risasi 10 ,Kisu kimoja, Bisibisi moja, Tiketi mbili za kusafiria kutoka Iringa hadi Makambako kwa kutumia basi la Lutengano, Bangi misokoto minne, Karatasi rizila na nguo mbali mbali za watu hao.

jeshi hilo limesema kuwa miili ya watu hao wanaosadikiwa kuwa ni majambazi imehifadhiwa katika hospital ya mji wa Makambako kwa uchunguzi, huku pia jeshi hilo likiendelea na upelelezi wa kumtafuta jambazi moja ambaye alikimbia katika eneo la tukio.

Video: Kishindo cha Magufuli kwa wafanyabiashara, PM aeleza maofisa wa TRA walivyodai rushwa
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Juni 8, 2019