Waziri wa Afya, nchini Kenya Mutahi Kagwe ametangaza visa tisa zaidi vya wagonjwa wa virusi vya corona nchini humo na kufanya kuwepo kwa watu 25 wenye virusi vya corona hadi kufikia Jumanne ya Machi 24, 2020.

Kagwe amesema kwamba kwa muda wa saa 24 zilizopita watu 82 walifanyiwa uchunguzi katika maabara ya KEMRI Kilifi na Aga Khan ambapo tisa kati yao walipatikana na virusi hivyo.

Wagonjwa hao ni kutoka kaunti za Nairobi, Mombasa, Kilifi na Kwale na miongoni mwa maambukizi hayo mapya ni Wakenya saba na raia wawili wa kigeni .

Ambapo wagonjwa wawili waliambukizwa baada ya kuchangamana na mwathirika wa virusi hivyo.

”Wagonjwa wawili walioambukizwa walisemekana kwamba walitangamana na mtu aliyekuwa ameathirika na virusi huku wengine wakiwa wasafiri kutoka nchi zingine ambazo zimeathirika, wagonjwa hao tayari wametengwa katika vituo vyetu vya afya na wanafanyiwa uchunguzi zaidi na wataalam wetu wa afya” amesema Waziri Kagwe.

Aidha Waziri ameongezea kuwa wameanza jitihada ya kuwasaka wale wote waliochangamana na wagonjwa hao ili waweze kuwachukua vipimo na kuwatenga karantini.

Waziri ametoa tangazo hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo ameandika.

”@MOH_Kenya Nine more people have tested positive of coronavirus from four counties, Nairobi Mombasa, Kilifi and kwale. Seven are Kenyans and two are foreigners #KomeshaCorona media briefing by Health CS, Mutahi Kagwe

 

 

 

Video: Makonda asema mtoto wa Mbowe ana Corona
Watanzania walia gharama hoteli za karantini, Waziri atoa muongozo