Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa limewakamata watuhumiwa 12 kwa makosa mbalimbali ya kiuhalifu ikiwemo wizi na utapeli wa uganga katika oparesheni maalumu inayoendelea mkoani hapo.

Akizungumza na waandishi wa Habari Kamanda Msaidizi wa Jeshi la Polisi Rukwa, ACP William Ampaghale amesema waganga hao wa kitapeli marufu kama lambalamba huwalaghai wananchi kuwa wana uwezo wa kuwaumbua wachawi wanaosababisha kutokupata mazao mazuri.

Vifaa vya uganga walivyokamata ni pamoja na kinu, mtwangio, mikuki miwili, shuka zenye rangi nyekundu na nyeusi, hirizi, kibuyu na madawa mbalimbali yakiwa katika ungo.

Katika hatua nyingine Jeshi hilo linawashikilia watu wanne waliokutwa na lita 75 za pombe ya Moshi pamoja na kete mbili za bangi, ambapo watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili.

Hata hivyo Kamanda Ampaghale amewaasa wanachi kushirikiana na Jeshi la Polisi endapo wanaona kuna kiashiria chochote cha uhalifu, na Wenyekiti wa vijiji kuacha kuwakaribisha waganga wa kienyeji na watu wasioeleweka.

Waziri Ummy asimamisha kazi watumishi wanne
Miaka 8 bila Ngwea