Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, kwa kushirikana na ofisi ya Taifa ya mashitaka limefanikiwa limefanikiwa kuwafikisha Mahakamani jumla ya watuhumiwa 270 kwa makosa ya ubakaji na watuhumiwa wawili kati yao wamefungwa kifungo cha maisha jela na wengine miaka 30 kila mmoja.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, iliyotolewa hii leo December 14, 2022 na Kamishina msadizi wa Polisi, Justine Masejo, imeeleza kuwa, kati ya watuhumiwa 270, 223 kati yao walipatikana na hatia na wawili ambao ni Peter Leonard (27) na Paul Hilonga (60), wamefungwa maisha jela kwa kosa la kubaka.
Amesema, Jeshi hilo liliendesha operesheni maaalum ambapo watuhuiwa 127 na pikipiki 125 zilikamatwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo taa mbazo zimepigwa marufuku, namba bandia na pikipiki ambazo zimefutwa namba ambazo zimemekuwa kero kwa wananchi.
Aidha, Kamanda Masejo ametoa rai kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi hilo ili kukomesha vitendo vya kihalifu huku akisemaJeshi hilo kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama wamejipanga vyema katika kuhakikisha sikukuu za mwisho wa mwaka zinakuwa za amani.