Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linaendelea na oparesheni iliyoanza toka Julai 1, 2021 ikiwa ni uthibiti wa uhalifu wa aina mbalimbali na ajali za barabarani.

Akizungumza na wandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani ACP Wankyo Nyigesa amesema kuwa kupitia opareshi hiyo wamefanikisha kuwakamata wahalifu 71, wanawake 20 na wanaume 51 wenye makosa mbalimbali ikiwemo wizi wa Kompyuta Mpakato, Gongo lita 92, Television, Magobole 2, Pikipiki 4, Bhangi puli 2, kete 122, msokoto 5 na vinginevyo.

Katika hatua nyingine Jeshi hilo la pwani pia limefanikisha kukamata sare za Jeshi la Wananchi ambazo zilikuwa zinatumika kinyume na sheria.

Kamanda ACP Wankyo, amesema kuwa upelelezi wa matukio hayo umeshakamilika na Jeshi la Polisi linataraja kupeleka majarada hayo kwa wakili wa serikali kwa kuandaa mashtaka dhid ya watuhumiwa hao

AIdha Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linaendelea kutoa rai kwa wananchi kushirikina na jeshi hilo kwa kutoa taarifa endapo watakuwa na shaka ya mtu huyo.

Ulega ataka sekta ya Mifugo kujiendesha kibiashara
Manara ataja kikosi bora VPL 2020-21