Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, amewasilisha muswada Bungeni na kusema kuwa  atakayetiwa hatiani kwa kosa la kusafirisha mirungi au bangi zaidi la kilo 50 atahukumiwa kifungo cha maisha gerezani.

Mapendekezo hayo ni kwa lengo la kudhibiti ongezeko la wafanyabiashara wakubwa wa madawa ya kulevya , kupunguza uuzaji na usambazaji dawa za kulevya.

Adhabu ya kifungo cha maisha gerezani, kwa mujibu wa muswada huo, ni kwa wanaowaweka rehani watu ili kufanikisha biashara ya dawa za kulevya, wamiliki wa mitambo ya kutengeneza dawa hizo na watakaowaingiza watoto kwenye matumizi na biashara ya dawa za kulevya.

Amesema masuala ya msingi yaliyozingatiwa kwenye muswada huo ni kuharamisha baadhi ya vitendo, kuweka adhabu, kuidhinisha vigezo vya kufuata wakati wa utoaji dhamana na uwezo wa mahakama katika kusikiliza mashauri yanayotokana na sheria hiyo.

Mhagama amesema kifungu cha 15(1) cha muswada huo kimependekezwa kuongezwa kipengele (C) ili kuweka katazo la kuwezesha au kusababisha mtu kusafirishwa nje ya nchi kuwekwa rehani ili kufanikisha biashara ya dawa za kulevya.

“Kipengele hiki kinaweka adhabu ya kifungo cha maisha kwa mtu atakayekiuka masharti ya kifungu hicho. Vilevile kifungu kidogo cha pili kimerekebishwa kwa kuzuia yeyote kujihusisha isivyo halali na kemikali zinazotumika kutengenezea dawa za kulevya.

Aidha amesema kuwa Kifungu cha 29, kimefanyiwa marekebisho kwa malengo ya kuongeza makosa yasiyostahili dhamana.

Kikosi cha Kilimanjaro Stars chatajwa
Tanesco: Upungufu wa umeme baadhi ya maeneo, jumamosi Novemba 18 na kesho Jumapili Novemba 19, 2017