Watu wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kula nyama za binadamu wanaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi nchini Afrika ya Kusini kitu ambacho kimepelekea kutupiliwa mbali ombi lao la kuomba dhamana.
Watu hao walifika mahakamani hapo wakiwa na lengo la kuomba dhamana kabla hata ya mahakama ya Estcourt kusikiliza tuhuma zinazowakabili watuhumiwa hao za kula nyama za binadamu nchini humo.
Aidha, Nje ya ukumbi wa mahakama hiyo , makundi mbalimbali ya watu na wanaharakati waliandamana kupinga kuachiliwa huru kwa washukiwa hao kwa dhamana kulingana na kosa linalowakabiri.
Miongoni mwa wanaokabiliwa na tuhuma hizo za kula nyama za binadamu ni pamoja na mganga wa jadi ambaye anatuhumiwa kuwarubuni wateja wake wale nyama za binadamu ili waweze kupata utajiri na kuwa na maisha mazuri.
-
Majaliwa aishukuru Cuba kwa kuthamini mchango wa mashujaa wa Afrika
-
Homa ya Nguruwe tishio nchini India
-
Rais aagiza polisi kuwaua wanaogoma kukamatwa
Hata hivyo, watu hao walikamatwa mara baada ya mmoja wao kwenda kujisalimisha katika kituo kimoja cha polisi kwa kuwaambia polisi hao kuwa amchoka kula nyama za binadamu.