Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Eliezer Feleshi amesema utafiti uliofanyika katika magereza ya Kusini mwa Tanzania, ilibaini kuna baadhi ya watuhumiwa ambao makosa yao yanadhaminika, wanafurahia zaidi kuendelea kubaki Mahabusu.

Dkt. Feleshi ameyasema hayo hii leo Julai 20, 2023 katika Kikao cha Wajumbe wa Tume ya haki jinai, DPC na Wahariri wa Vyombo vya Habari Ikulu jijini Dar es Salaam.

amesema Tume ya Haki Jinai pia imependekeza viongozi wa umma wanaotumia vibaya madaraka yao kuwaweka mahabusu wananchi kinyume cha sheria, washtakiwe binafsi mahakamani badala ya kuishirikisha Serikali.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki Jinai, Balozi Ombeni Sefue, alisema mapendekezo yaliyotolewa kuhusu uboreshaji mfumo wa haki jinai, yatafafanyiwa kazi kutokana na utashi wa kisiasa wa Rais Samia Suluhu Hassan na utekelzaji wake unategemea hali ya uchumi.

Mamlaka Wakuu wa Mikoa, Wilaya yanatumika vibaya
Manchester United yaichorea mstari Atalanta