Kufuatia uhalifu mbalimbali unaofanyika kwa njia ya simu Taasisi husika ikiwemo TCRA, mashirika ya mawasiliano kwa kushirikiana na jeshi la polisi imefanya jitihada mbalimbali kuhakikisha wanadhibiti uhalifu huo.
Tahadhari hizo ni pamoja na kutoa elimu kwa wananchi juu ya matumizi sahihi ya simu pamoja na namna ya kukabiliana na wahlifu hao wanaotumia simu za mkononi kufanya miamala isiyo ya uhalali na utapeli mwingine.
Hivyo basi jeshi la polisi limetoa tahadhari zifuatavyo ni katika kuhakikisha simu zinatumiwa kwa munufaa na si vinginevyo, hivyo imewataka wananchi kuchukua tahadhari hizi.
- Usinunue simu za Android kwa mtu usiyemjua. Hiyo ni hatari kwani hujui hiyo simu imetolewa wapi, inawezekana ukapewa kesi ya wizi au mauaji endapo simu hiyo ilikuwa imeibiwa kwa mtu aliyeuawa, chukua tahadhari.
- Unapoiona line ya simu njiani ipo chini usiokote na kuiweka kwenye simu yako ili kujua ina salio kiasi gani na ujihamishie, ni hatari.
- Usimpe mtu usiyemjua simu yako apige sehemu yeyote, hiyo ni hatari sana wengi wameibiwa simu na mali zao kama fedha kwa namna hiyo, chukua tahadhari.
- Simu inapoibiwa au mwenye simu kuuawa, line hutupwa, unapoiweka simuni mwako simu yako inahusishwa na tukio hilo.
- Unapoweka salio, hakikisha karatasi ya vocha unaichana, umapoitupa watu wanaweza kufanya mauaji wakachukua karatasi ya vocha ile na kuweka sehemu ya tukio au pale ulipoitupa kukatokea tukio na wewe ukahusishwa.
- Usikubali kumsajilia mtu line yake kwajina lako hata kama mtu wako wa karibu sana, baba, mama, dada au kaka.
- Kumbuka namba yako umesajiliwa, moja ya matukio hayo yakitokea na namba yako kuonekana moja kwa moja unakuwa mtuhumiwa namba moja.
- Wengi wamepewa kesi za mauaji, wizi bila kujua, polisi wapo kazini wanapoona vidhibiti wanachukua kwani hawatojua kama umehusika au hujahusika.
Hivyo wananchi na watu wote wanaotumia simu wanapswa kuwa makini ili wasijekujikuta wameingia matatizoni kwani sheria za mtandaoni sasa zinafuatwa kwa hali ya juu.