Watumiaji wa bidhaa za kampuni ya Apple duniani wamecharuka baada ya kusikika tetesi kuwa kuna mabadiliko katika toleo jipya la siku za iphone (iPhone 7) kuwa haitakuwa na kitundu cha kuweka ‘earphones’.

Kwa mujibu wa tetesi hizo, toleo hilo la iPhones 7 litakuwa na earphones zitakazounganishwa kwenye simu kwa njia ya Bluetooth.

iPhone earphones

Watumiaji wa bidhaa hiyo zaidi ya 227,000 wamepinga kwa kutia saini kwenye pingamizi lililowekwa kwenye mtandao wa sumofus.org, lenye kichwa cha habari “Apple is ditching the standard headphone jack to screw consumers and the planet.”

Sababu kubwa iliyopelekea watumiaji hao kupinga kwa nguvu toleo hilo, ni kuwa kutokuwa na ‘kitundu’ cha kuweka earphones kutapelekea earphones walizonunua katika matoleo yaliyopita kutokuwa na kazi tena.

Mshindi Wa Tuzo Ya Dunia Kujulikana Leo
Thomas Ulimwengu Aeleza Anavyojiandaa Kwenda Ulaya