Watumishi watatu wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro na Mawakala watatu wanaotumika katika ukusanyaji wa ushuru wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kufoji mashine ya kukusanyia mapato isiyotambulika katika mfumo wa ukusanyaji wa mapato ya halmashauri.
Akithibitisha kuwepo kwa ubadhilifu huo katika kikao cha Bajeti cha kamati za madiwani, Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Alhaji Majid Mwanga amewataka watumishi wa halmashauri kuacha tabia za kutengeneza mitandao ya wizi wa fedha za serikali na kuwaonya watumishi yakuwa, Serikali ya awamu ya sita haitoshindwa kuwachukulia hatua za kinidhamu na kisheria kwa wale watakaobainika kuhujumu mapato ya halmashauri.
Kwaupande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilosa Wilfred Sumari anafanunua hatua za kinidhamu zilizochukuliwa kwa watumishi hao, huku Diwani wa kata ya Dumila akifafanua namna wizi huo ulivyokua ukifanyika.