Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima amewasimamisha kazi watumishi watano wa hospitali ya Wilaya ya Nansio Ukerewe kupisha uchunguzi baada ya kudaiwa kufanya ubadhirifu na wizi wa dawa yenye thamani ya milioni 200.

Watumishi hao wamesimamishwa kazi kuanzia leo Januari 19, 2021 ili kupisha uchunguzi wa vyombo vya maadili ya utumishi wa umma pamoja na maadili ya mabaraza na bodi za kitaaluma, kufuatia ubadhirifu uliobainika wakati Dkt. Gwajima alipofanya ziara katika hospitali hiyo hivi karibuni.

Watumishi hao sita wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma za wizi wa dawa za zaidi ya Shilingi 200 Milioni ambapo mmoja wao alikiri na kuhukumiwa kulipa Milioni 100 na waliobakia wamerejeshwa kazini.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Cornel Maghembe amemueleza Waziri Gwajima kuwa hajaridhishwa na watumishi hao kurejeshwa kazini kwani hawaaminiki tena.

Mara baada ya Gwajima kutembelea hospitali ya Nansio alijionea kuendelea kuwepo kwa viashiria vya udanganyifu katika mfumo mzima wa ugavi wa dawa hivyo kukubaliana na maelezo ya Magembe kuwa bado kuna tatizo kama alivyoeleza.

Aidha, Gwajima amemuagiza Mkurugenzi wa Wilaya ya Ukerewe, Esther Chaula kuwasimamisha kazi watumishi hao na kuwafikisha kwenye kamati ya maadili ya utumishi wa umma, mabaraza na bodi za kitaaluma na vyama vyao ili kubaini kama kweli hao watumishi bado wanastahili kuaminika tena kwa mujibu wa sheria za utumishi wa umma, mabaraza na bodi za kitaaluma pia maadili ya vyama vyao vya kitaaluma.

Saa za Trump White House zayoyoma
Tanzania, Uingereza 'pasu kwa pasu' mkataba wa madini