Watumishi wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wametakiwa kuimarisha mifumo ya utendaji kazi ikiwemo kutatua changamoto zinazowakabili watanzania ili kuweza kuleta taswira bora na maendeleo kwa taifa.

Naibu Katibu Mkuu Elimu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Gerald Mweli ameyasema hayo katika ofisi za TAMISEMI Jijini Dodoma kufuatia mapokezi aliyoyapata kutoka kwa watumishi wa wizara.

Amesema ili kufikia matokeo bora ya kuwatumikia watanzania ipo haja ya kuimarisha ushirikiano katika utendaji wakazi na jamii wanayoihudumia kwakuwa hiyo ni dira ya waliyonayo katika nafasi zao za kazi.

“Ili kufanikisha utendaji bora wa kazi lazima kila mtu ajipime katika utendaji wake kwa kujituma na kuhakikisha utendaji wake huo wa kazi unaleta matokeo chanya kwa taasisi na taifa na unapokuja kwangu na tatizo juu ya kukosoa njoo na suluhisho nini kifanyike ili kufikia malengo,” amesema Mweli.

Ameongeza kuwa watendaji wake wanatakiwa kuhakikisha wanakaa pamoja na kutatua changamoto ya madeni ya walimu kama alivyo elekeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kalipo kuwa anawaapisha Viongozi wapya Ikulu Jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Elimu Dkt. George Jidamva akiongea katika ukaribisho huo amezielezea Idara zilizopo chini ya Idara ya Elimu katika Ofisi ya Rais TAMISEMI sambamba na kuainisha majukumu ya Sekta ya Elimu.

Naye  Mkurugenzi wa Idara ya Utumishi Ofisi ya Rais TAMISEMI Victor Kategere amesema watumishi wote wako tayari kushirikiana naye na kuhakikisha wanaleta matokeo chanya katika utendaji kazi.

Mweli anachukua nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Elimu TAMISEMI Mathias Kabunduguru aliyeteuliwa kuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania kufuatia uteuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Magufuli uliofanywa hivi.karibuni.

Abdelkarim Hassan atupwa jela ya soka, FIFA yaingilia kati
Mbappe avunja rekodi ya Lionel Messi