Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Dkt. Lauren Ndumbaro amewataka wakurugenzi, wakuu wa idara na watumishi wote kuwa wazalendo na kuwatumikia vyema wananchi.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa umma wa manispaa ya Songea, ambapo amesema kuwa ni lazima kila mtumishi atimize majukumu yake ili kurahisisha majukumu ya mwingine kwani idara nyingi zinategemeana kiutendaji.

“Kila mtumishi inabidi ajitathimini abadilike awe mwadilifu zaidi, awe mchapakazi zaidi, awe binadamu zaidi na awe mwaminifu zaidi,”amesema Ndumbaro.

Hata hivyo, Ndumbaro amewataka Wakurugenzi na Maafisa utumishi kushughulikia na kuyatatua matatizo ya watumishi na endapo hawatafanya hivyo basi wizara itasimamisha mishahara yao ili nao wapate usumbufu kama wanaopata watumishi wa kawaida.

Trump, Putin kuliangamiza kundi la IS
Diamond afunguka ujio wa ngoma yake na Rick Ross