Wakaguzi wawili wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), katika halmashauri ya wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro wamefukuzwa kazi kwa tuhuma za kupokea rushwa sh. 50,000, kutoka kwenye kiwanda cha Mashati Oil Investment Limited.

Wafanyakazi waliokutwa na mkasa huo ni aliyekuwa mratibu wa shughuli za TFDA na Ofisa Afya wa wilaya ya Rombo, James Merisho pamoja na Ofisa Mazingira na taka ngumu wa wilaya hiyo, Mathias Gungumka.

Taarifa iliyotolewa na TFDA imeeleza kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya mamlaka hiyo kupokea taarifa kutoka Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kuwa viongozi hao wanatuhumiwa kuhusika na vitendo vya rushwa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wakaguzi hao hadi sasa wameondolewa katika orodha ya wakaguzi wanaotambulika na TFDA.

“Wahusika hawaruhusiwi kufanya kazi za TFDA tena na kwamba yeyote atakayewaona wakifanya kazi kwa vitambulishao vyao atoe taarifa ofisi za kanda TFDA au kituo cha Polisi,”imesema taarifa hiyo

Hata hivyo, TFDA imewaonya wakaguzi wake wote kutojihusisha na vitendo vya rushwa na kwamba haitavumilia mtumishi yeyote anayejuhusisha na vitendo hivyo.

 

 

Serikali kuzifanyia mapitio upya Leseni za uchimbaji madini
Kufanya Kazi Ukiwa Likizo: Njia 5 za Kufanikiwa