Watu waliojihami kwa silaha wamewaua waumini saba wa dini ya Kiislamu na kuwajeruhi wengine watatu katika mashambulizi mawili tofauti katika jimbo la Kaskazini Magharibi mwa Nigeria, Kaduna.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Polisi, Mansir Hassan amesema watuhumiwa wa magenge ya uhalifu waliwarushia risasi waumini wa jamii ya Saya-Saya wakati wa swala na kusababisha vifo vya watu sita.

“Wahalifu hao tisa walifika eneo la tukio wakiwa kwenye Pikipiki na kuanza kuwashambulia watu Msikitini. Baadae walielekea kwenye kijiji jirani na kushambulia msikiti mwingine na kumuuwa mtu mmoja ambapo pia watu watatu walijeruhiwa,” amesema Mansir.

Kaduna, ni moja kati ya majimbo ya Kaskazini magharibi na kati mwa Nigeria ambayo yanakabiliwa na vitisho vya majambazi wanaovamia vijiji, kuua na kuteka nyara raia.

Ajali nyingine Morogoro: Yauwa, yajeruhi
Ukatili: Wanawake, Watoto wahanga wakuu