Waumini wa Kanisa la Anglikani Njombe mjini wameungana na wakristo wengine nchini Tanzania na Duniani kote kuadhimisha Sikukuu ya kufufuka kwa yesu Kristo (Pasaka) 2019, Misa maalumu ya kuadhimisha Sikukuu hiyo iliongozwa na Padri Silvester Msigwa.

Akizungumza na mamia ya waumini wa Kanisa Anglikani mjini Njombe waliohudhuria misa hiyo takatifu ya ufufuo wa Yesu Kristo Mchungaji Silvester Msigwa ametoa wito kwa wakristo wa kanisa hilo kuishi maisha ya kumpendeza Mwenyezi Mungu kwa kuacha matendo mabaya na kufuata njia za kumpendeza Kristo.

“Wakristo wenzangu tunapo sherehekea sikukuu hii ya pasaka tunatakiwa kuacha matendo yetu mabaya na kuishi katika matendo yanayo mpendeza mwenyezi Mungu ambae alimtoa mwanae mpendwa Yesu Kristo ili aje Duniani kutukomboa sisi wanadamu,”amesema Msigwa.

Amewataka waumini wa Kanisa Anglikani na Watanzania wote nchini kuitumia sikukuu hiyo ya Pasaka kuliombea Taifa na Viongozi wake wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ili kwa uwezo wa Mungu wazidi kuwatumikia Watanzania kwa Amani.

Amesema kuwa Serikali imeendelea kuboresha maisha ya wananchi kwakuimarisha miundimbinu mbalimbali ikiwemo Afya, Maji, Barabara, Elimu na Sekta nyingine hivyo wananchi wanatakiwa kushukuru hata kwa kidogo ambacho serikali inatoa na kumuomba Mungu azidi kuwaongezea Maarifa ya kiutendaji viongozi wa Taifa la Tanzania.

Wakizungumza mara baada ya kuhitimisha Misa hiyo takatifu ya Pasaka Baadhi ya waumini walioshiriki wamesema kuwa Sikukuu hiyo ni kumbukumbu maalumu ya maisha ya Yesu Kristo akiwa Duniani ambae aliishi maisha ya kumpendeza Mungu hata alipoamua kunyenyekea hadi mauti yalipomkuta hivyo nao wameendelea kuyaenzi na kuishi maisha hayo.

 

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Aprili 22, 2019
Arusha: Asimulia alivyohama ghafla kwenye gari iliyopata ajali, RPC azungumza